May 8, 2013



Julio wa kwanza kushoto, akiwa na meneja Moses Basena, kocha wa makipa James Kisaka na Daktari Cosmas Kapinga wakiwajibika katika moja ya mechi za Ligi Kuu Bara wakati Simba ikipambana..

Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo maarufu kama Julio amewadhihaki mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga kwamba hawana tofauti na mti wa mwembe ulio uani.

Julio ambaye ni beki wa zamani wa Simba, amesema anaamini kikosi chao kinachoundwa na vijana wengi kitacheza na kuwafunga Yanga katika mechi yao ya Mei 18.

Alisema tofauti na wengi wanavyoamini, kikosi chao kimeweza kucheza vizuri katika mechi ya leo na kuifunga Mgambo ambayo ilitoka sare ya bao 1-1 na Yanga na kuizuia kutangaza ubingwa.


“Nakuambia hao Yanga hawana tofauti na mwembe wa uani, unatingisha unakinga kapu lako unachukua matunda.

“Unajua watu hawajui, lakini niamini Yanga ni timu laini sana na hawana uwezo wa kunifunga mimi.

“Tokea nikiwa mchezaji au kocha nimekuwa nainyanyasa Yanga ninavyotaka, utaona siku ikifika,” alijigamba Julio.

Julio alisisitiza kwa kuwa wameishajihakikishia kushika nafasi ya tatu, basi watacheza na Yanga kushinda na kujiwekea heshima.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu huku Yanga wakisisitiza kuwa wanataka kushinda ili wapokee kombe lao kwa furaha zaidi.

Msimu uliopita, Simba ikiwa tayari imeishatwaa ubingwa, iliichapa Yanga kwa mabao 5-0 na kuweka historia ya mabao mengi ikifuatia ile ya ushindi wa 6-0 walioshinda Simba katika miaka ya 1970.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic