May 8, 2013

 
Saa chache baada ya Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson kutangaza kujiuzulu mwisho mwa msimu huu, mshambuliaji wa Real Madrid ametoa shukurani zake.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Ronaldo amendika: “Thank you for everything Boss”.

Hali ambayo ilionyesha ni moja kwa moja alikuwa akituma shukurani zake kwa kocha huyo maarufu kama Boss.




Ferguson ndiye alimtoa Ronaldo katika klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno na kumpa majukumu mazito akiwa na umri usiofikia miaka 20.

Pamoja na kupata mafanikio makubwa akiwa na United hadi kufikia kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2008, Ronaldo ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi kubwa ya mauzo ya pauni milioni 80 aliyoiweka akitokea Man United kwenda Real Madrid.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic