Frank Lampard amefunga bao lake la 202 na 203 kwa Chelsea
na kumvuka Bobby Tambling aliyekuwa anashikiria rekodi ya ufungaji wa mabao
mengi katika klabu hiyo.
Pamoja na kufunga mabao hayo katika mechi ya Aston
Villa na kuvunja rekodi hiyo, Lampard ameigakikishia Chelsea nafasi ya kucheza
Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kufikisha pointi 72 ingawa Arsenal
wanaonekana kutokata tama.
Baada ya mechi hiyo, Lampard alizungumza na
Tambling kuhusiana na suala hilo la rekodi.
Pamoja na kuvunja rekodi ya Tambling, kiungo huyo
mkongwe wa Chelsea anashikilia rekodi ya kuwa kiungo mwenye mabao mengi zadi
katika Ligi Kuu England.
ANGALIA LISTI YA VIUNGO WENYE MABAO MENGI PREMIER..
Frank Lampard – 165
Ryan Giggs – 109
Paul Scholes – 107
Matthew Le Tissier – 100
Steven Gerrard – 98
0 COMMENTS:
Post a Comment