May 10, 2013



 

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts aliifuatilia Simba kwa umakini mkubwa wakati inaivaa Mgambo shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Brandts, daftari na kalamu mkononi akiwa na daktari wa timu hiyo Nassor Matuzya na msemaji, Baraka Kizuguto, Brandts raia Uholanzi alionekana kuuliza maswali na kutaka kujua mambo mengi kuhusiana na Simba.

Hata hivyo, kikosi cha Simba kilichocheza siku hiyo kilikuwa kimepumzisha wachezaji zaidi ya wanne ambao watacheza dhidi ya Yanga.

Tayari Brandts ameanza kuonyesha hofu dhidi ya Simba iliyo chini ya Mfaransa, Patrick Liewig. Simba na Yanga zinakutana Mei 18 katika mchezo wa mwisho wa kufunga ligi ambao zaidi umelenga kulipa kisasi kwa Yanga na kuendeleza ubabe na kulinda heshima kwa Simba pia ambayo msimu uliopita ilifunga msimu kwa kuichapa Yanga bao 5-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic