May 9, 2013



Kocha Mkuu wa TP Mazembe, Lamine Ndiaye ameamua kubwaga manyanga ikiwa ni siku chache baada ya timu yake kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtanzania, Mbwana Samatta ni kati ya washambuliaji tegemeo katika kikosi cha TP Mazembe, pia Thomas Ulimwengu na wote wako katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

TP Mazembe ilitolewa baada ya kushinda mechi yake ya pili kwa bao 1-0 wakati ilitakiwa kushinda 2-0 dhidi ya Orlando Pirates  ya Afrika Kusini kwa mabao 3-1 jijini Johannesburg.
Ndiaye raia wa Senegal ameamua kutangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo baada ya kutolewa kwa michuano hiyo na sasa imepangwa kushiriki Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Msumbiji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic