Kocha Mkuu
wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Pitso Mosimane ameshangazwa kusikia
kiungo wa zamani wa Simba, Selemani Matola hadi leo hana timu anayoifundisha.
Mosimane
aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Supersport United, ameiambia Salehjembe ambakuwa
akitaka kujua kuhusiana na Matola ambaye anaamini ni kati ya viungo bora
aliowahi kuwaona.
“Mchezaji
akiwa na uwezo wa kuiongoza timu uwanjani wakati akicheza, ujue ana nafasi
kubwa ya kuwa kocha bora.
“Tokea
akiwa anacheza chini yangu, niliamini Matola angekuja kuwa kocha bora kabisa. Lakini
kama sasa hana timu, huenda hapendi kufanya kazi ya ukocha,” alisema Mosimane
kutoka Afrika Kusini.
“Niliwahi
kumuambia, unajua wakati anacheza kwamba anaweza kuwa kocha, anajua kubadilisha
mpira na wakati gani afanye hivyo na timu icheze,” alisema Mosimane.
Wakati akiwa
kocha Supersport, Mosimane alimsajili Matola hata bila ya kumfanyia majaribio
baada ya kuiongoza Simba kutwaa Kombe la Tusker jijini Nairobi kwa kuifunga
timu yake bao 1-0 na Hearts of Oak kwa mabao 4-2.
Matola alikuwa
kocha wa timu ya vijana ya Simba aliyoisaidia kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na
kutwaa Kombe la BancABC.
Lakini
baadaye alikorofishana na uongozi wa Simba chini ya Ismail Aden Rage na kuamua
kuachia ngazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment