Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa
vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto
wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa
na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano
(roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na
kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua
inayofuata.
Hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa)
ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa na fedha
likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.
Vifaa na fedha zitapatikana wakati
wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo
vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania.
Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na
mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca
Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa
yakifanyika kila mwaka.
BONIFACE WAMBURA
MSEMAJI TFF
0 COMMENTS:
Post a Comment