Mlezi wa
Simba, Rahma Al Kharusi amefanya kazi ya ziada kumshawishi mmiliki wa
Sunderland kukubali kuisaidia klabu hiyo.
Katika mazungumzo
kati ya Ellis Short, bilionea mmiliki wa Sunderland na Rahma maarufu kama Malkia
wa nyuki, mafanikio yamekuwa makubwa sana.
Ingawa Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage aliongozana na mwanamama huyo, lakini ushawishi
mkubwa ulitoka kwake.
Kwani ndiye
aliyetoa maombi ya wachezaji kupata nafasi ya kufanya majaribio Sunderland,
makocha wao kujifunza na pia kuanzishwa kwa Academy.
Short
amekubali mambo yote kimsingi, maana yake ni suala la Simba kuitumia vizuri
nafasi hiyo waliyoipata kwa ushawishi wa mwanamama huyo mwanamichezo.
Simba
imeruhusiwa kupeleka wachezaji kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa
katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.
Ukichana na
hivyo, itapata fursa ya kujengewa uwanja wa mazoezi ambao zaidi utatumiwa na
timu za watoto kuanzia miaka mitano hadi 11 na baadaye hadi chini ya miaka 16.
Kupitia Sunderland
na maombi yaliyotolewa na Malkia wa nyuki maana yake, Simba ndiyo watafaidika
zaidi kwa kuwa na urafiki na klabu hiyo.
Huenda
kutotanguliza fedha kwanza kama msaada namba moja kumeisaidia Simba kupata
mambo yote hayo.
Kwani kama
yatatumika vizuri, maana yake yanaweza kuisaidia klabu hiyo kupata fedha nyingi
zaidi hapo baadaye.
Huenda kikaonekana
ni kama kitu kidogo tu, lakini alichokifanya Malkia wa nyuki si kitu kidogo na
kinatakiwa kulindwa vilivyo.
Kukilinda kwake
ni watu kufanya utekelezaji bila ya kuvunja makubaliano na wazungu hao, kwani
kama watakiuika, basi ndiyo utakuwa mwisho wa makubaliano na hasara itabaki
kuwa kwa Simba.
Lakini kama
wataitumia nafasi hiyo vizuri, itakuwa ni faida kubwa lakini wataonyesha
wameelewa alichokitaka Malkia wa nyuki ambaye ameangalia mbele zaidi badala ya
fedha kwa ajili ya leo pekee bila ya kujua kesho ukiamka utajiendesha kwa
kutumia fungu lipi.
Huenda Malkia
angebaki kwake na kuendelea na biashara zake, au kujumuika na familia yake
lakini amekubali kusafiri maelfu ya kilomita kwenda kuipigania Simba huko England.
Hakika ni
kitu cha kumpongeza, lakini itakuwa faraja kwake kama makubaliano hayo
yatatumiwa vizuri na uongozi wa Simba.
Iwapo longolongo
itaingia katikati, kwanza kabisa itakuwa ni kumkatisha tamaa kwa kiasi kikubwa
na huenda ataanza kukumbuka hasi, kwamba alipoteza muda wake.
Pili,
mtamuabisha, maana alichokiomba hakitafanyika na mwisho itaonekana yuko kwenye
kundi lenu la kubahatisha.
Makubaliano
ya uhusiano na Sunderland si kitu kidogo kwa kuwa imepiga hatua tena mbali kwa
maendeleo ya soka na Simba imepata bahati ya mtende. Vema ikaitumia kwa manufaa
ya klabu na si wajanja wachache wanaojua kuzungusha maneno mdomoni, huku mikono
yao inachota mali za klabu.
Simba hiko vizuri sana , sasa hapo fitina na majungu ziwekwe pembeni watu wafanye maendeleo
ReplyDeleteShe is a lady of deeds than words she deserves our thanks for her vision and to care for the development of others.
ReplyDeleteNimeipenda hii. Well done Malkia wa Nyuki!
ReplyDelete