Kocha mwenye vituko, Jose Mourinho amewaambia
waandishi wa habari wa shirika la Sky Sports la Uingereza kwamba Alex Ferguson
ni rafiki yake mkubwa na anajua atakwenda timu gani baada ya kuondoka Real
Madrid.
Mourinho raia wa Ureno amesema alikutana na
Ferguson na akamueleza kwamba atastaafu kitu kilichomshitua sana na alikuwa
kati ya watu waliojua mapema suala hilo.
“Ulikuwa ukienda kucheza Old Trafford unaanza
kumfikiria Ferguson kuliko timu utakayocheza nayo, aliponiambia nilishtuka
sana. Hakikuwa kitu kilichokifikiria na ilinichukua muda kuamini.
“Yeye pia anajua baada ya Madrid nitakwenda wapi,
tunabadilishana mawazo kuhusu mambo mengi tu kwa kuwa sisi ni marafiki wa
karibu.
“Kuhusu Moyes, nafikiri ni mtu sahihi kabisa na
atapata mafanikio makubwa akiwa na Real Madrid. Mambo mengi anafanana na
Ferguson na kazi yake ni nzuri, muda utatoa majibu lakini vizuri wakamuamini.
“Uamuzi wa Ferguson umekuwa ni sahihi na katika
wakati mwafaka na anastahili kula maisha kwa utulivu kwa kuwa amefanya kazi
kubwa,” alifunguka Mourinho.
Awali kulikuwa na taarifa Mourinho angepewa kazi ya
kuinoa Manchester United baada ya Ferguson kutangaza kustaafu mwishoni mwa
msimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment