May 11, 2013




Kocha wa Barcelona, Tito Vilanona amefunguka na kusema wachambuzi wengi wamekuwa wakiangalia namna Barcelona ilivyoshindwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kudhani imeporomoka.

Lakini wameshindwa kueleza namna kikosi chake kilivyoweza kuianguisha katika La Liga, Real Madrid yenye kikosi bora zaidi tokea ianzishwe.

Katika mahojiano mjini Barcelona, Vilanova alisema msimu uliopita, Real Madrid ilichukua ubingwa kwa kufikisha pointi zaidi ya 100 ikiwa chini ya Kocha Mreno, Jose Mourinho, awali hakukuwa na kikosi kilichofikisha pointi hizo katika timu hiyo.

“Lakini utaona msimu huu tumefanya vizuri sana na kuwapita mbali, ubora wetu wa msimu huu umezuia kufanya vizuri kama walivyotegemea au kama walivyofanya msimu uliopita.

“Kama ukisema ligi ya mabingwa, wote tumefeli, lakini kutofika fainali haina maana hatukuwa bora. Tumeteleza na tunaweza kujirekebisha, kusema Barcelona imekwisha ni makosa,” alisema Vilanova.

“Bado kikosi change kina wachezaji bora kabisa, sipendi wavunjwe moyo kwa kutofanya vizuri katika mechi mbili tu. Wamefanya vizuri mfululizo, wanapaswa kupongezwa na kupewa kile wanachostahili.”

Wadau wengi wamekuwa wakielezea mara kwa mara kwamba Barcelona imeonyesha kupoteza mwelekeo kutokana na kutolewa na Bayern Munich katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuchapwa jumpa la mabao 7-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic