May 12, 2013



Manchester United imeanza mikakati kwa ajili ya usajili mpya wa msimu ujao na imemlenga mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema kuzipa pengo la Wayne Rooney.

Man United ambayo itakuwa chini ya Kocha David Moyes kuanzia msimu ujao inasubiri kujua kama Rooney ataondoka kwa kitita cha pauni milioni 25, halafu yenye ianze kupambana kumpata Benzema kwa pauni milioni 30.

Bosi huyo mpya, inaonyesha hana uhusiano mzuri na Rooney wakati wakiwa wote Everton na Rooney alielezea katika kitabu kinachohusu maisha yake.

Lakini kumekuwa na taarifa kwamba Rooney angependa kufanya kazi na Moyes ambaye alimpa nafasi ya kucheza Premiership kwa mara ya kwanza wakiwa Everton, wakati huo mshambuliaji huyo alikuwa na miaka 16 tu.

Hata hivyo, pamoja na Rooney ,27, kuwa ameomba kuondoka, kuna taarifa kwamba Moyes ndiye atakuwa na kauli ya mwisho kuhusiana na suala hilo. Lakini pia uongozi wa Man United utasubiri aamue kuhusu Benzema.

Bado kuna taarifa za Rooney kuwania na timu kadhaa na Paris Saint-Germain, Bayern Munich na Chelsea ndiyo zimekuwa zikionyesha zitanaka huduma yake.

Mfaransa Benzema, 25, amebakiza mkataba wa miaka miwili na Madrid aliyojiunga nayo mwaka 2009.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic