May 9, 2013




Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ amekatwa Sh 50,000 katika mshahara wake kutokana na kuchelewa kufika mazoezini.

Wiki iliyopita, wachezaji wawili wa Yanga, Simon Msuva na David Luhende walikatwa mshahara kutokana na uamuzi wao wa kwenda kucheza mechi za mtaani maarufu kama ndondo.


“Chuji amekatwa mshahara wake baada ya kuchelewa kufika mazoezini.
“Huo ndiyo umekuwa utaratibu siku hizi na benchi la ufundi la Yanga sasa halitaki mchezo,” kilieleza chanzo cha uhakika.

“Kawaida wachezaji hukatwa shilingi elfu ishirini lakini ilipitishwa Chuji akatwe zaidi kwa kuwa mfano kwa vijana.

“Ingawa alilalamika, lakini uamuzi huo ulipitishwa na kocha mkuu Brandts aliungana nao.”

Yanga chini ya Brandts imekuwa ikitaka wachezaji wake kuishi kwa kujali zaidi mazingira ya kazi yao badala ya kufanya mambo ‘kiswahili’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic