May 9, 2013





Unaweza kumekucha, mashabiki wa Real Madrid wameonyesha wazi kwamba wamemchoka kocha wao, Jose Mourinho.

Mashabiki hao wamemzomea Mourinho wakati akitambulishwa wakati timu hiyo ilipokuwa inaivaa Malaga kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.


Lilipotajwa jina lake wakati amsogelea kocha wa Malaga kumsalimiia, karibu nusu ya mashabiki uwanjani hao walizomea kwa kupiga kelele.”boooooooo”.


Mourinho alinekana kutojali, ingawa alishindwa kuficha machungu yake kupitia usoni baada ya mashabiki hao kumshangilia kwa nguvu kipa Iker Casillas aliye katika ugomvi na kocha huyo Mreno.

Wakati Casillas alipotambulishwa, mashabiki hao walisimama na kuanza kumpigia makofi wakionyesha heshima kwake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic