May 24, 2013



 
Mashabiki wa timu ya TP Mazembe wamempachika mshambuliaji wao, Mbwana Samatta jina la shetani.

Samatta amekuwa akijulikana kwa jina la El Diablo, ikiwa na maana ya shetani kwa lugha ya Kihispania.

Pamoja na mashabiki, mitandao mbalimbali ya DR Congo inaonyesha kulikubali jina hilo la Samatta kwa kuwa imekuwa ikilitumia.


Mmoja wa mtandao maarufu wa DR Congo, uliripoti kwamba mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi naye alimuita Samatta kwa jina hilo la El Diablo na kusababisha wachezaji wengine wacheke.

Mganda, Emmanuel Okwi, naye alibandikwa jina la “mtoa roho” na mashabiki wa Simba, wakilinganisha uwezo wake uwanjani na alivyokuwa akisababisha vilio wka timu nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic