Saanya (katikati)... |
Mwamuzi Martin Saanya aliyepewa ‘ulaji’ wa kuchezesha mechi ya watani
Simba v Yanga keshokutwa Jumamosi, sasa hapokei simu hata upige kwa ‘namba ya
rais’.
Saanya anayetokea Morogoro, amegoma kabisa kupokea simu yake ya
kiganjani na mara nyingi imekuwa ikiita tu.
Baadhi ya wadau wameiambia Salehjembe kwamba kutopokea kwake simu ndiyo
salama yake kwa sababu anataka “kuepusha” maneno.
“Unajua mechi ya Simba na Yanga ina maneno sana, mimi nimewahi
kuchezesha. Hakika unakuwa huna amani hadi ipite na wakati mwingine hata
ikipita hakuna amani, lawama lazima kutoka upande mmoja au pande zote,” alisema
mmoja wa waamuzi wa zamani ambaye hakutaka kutajwa jina.
“Inawezekana ndiyo maana Saanya hataki kupokea simu maana akipokea tu,
kuna mtu anaweza kusema alizungumza naye na mambo ni safi. Watu wengi wa mpira
ni tatizo.”
Salehjembe nayo iliamua kujaribu kwa kupiga zaidi ya mara sita simu ya
Saanya ambayo iliendelea kuita bila ya mafanikio.
Saanya amepewa nafasi hiyo baada ya TFF kumbadili mwamuzi Israel Mujuni
Nkongo hali ambayo imefanya Simba itishie kususia mchezo huo.
Hana lolote huyo, wanafikiri hatujui jinsi wanavyochukuaga hela? Matajiri waga wanawatumia jamaa zao wa karibu sana kupitisha mlungula, unafikiri wanaongea nae yeye kwenye simu, la hasha! mzigo unapitia kwa mtu mwingine kabisa anayekutana nae kila siku, anaweza kuwa ndugu au rafiki yake wa karibu sana
ReplyDelete