Fainali ya Jumamosi ya Copa del Rey ni gumzo kwa kuwa ni mechi
inayowakutanisha wapinzani wakubwa wa soka la Hispania.
Real Madrid na Atletico Madrid wanaotokea katika jiji moja, lakini
inaonekana kuina kazi kubwa kwa kuwa Atletico ni mabingwa wa fainali na Madrid
chini ya Jose Mourinho wanapaswa kujipanga sawasawa.
Atletico Madrid wameshinda mechi nne katika fainali tano walizocheza
kuanzia mwaka 2010, hali inayowafanya waonekane ni hatari katika hatua ya
fainali wanapopata nafasi.
Maana yake, Real Madrid wanapaswa kuwa makini na wepesi kung’amua
mipango ya Atlerico Madrid ambayo wachezaji wake.
Ingawa wengi wanatupa jicho kwa Real Madrid ambayo haina kombe na
itatumia nguvu zote kulipata la Copa del Rey, lakini utaalamu wa Atletico
Madrid katika fainali unaonekana ni tatizo kwao.
0 COMMENTS:
Post a Comment