Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche ameweka rekodi ya kuwa raia wa kwanza wa Ivory Coast kuibuka mfungaji bora Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hiyo ni rekodi mpya katika Ligi Kuu Tanzania bara kwa mchezaji raia wa nchi iliyo Afrika Magharibi kuibuka mfungaji bora.
Awali Wakenya, Waganda wamewahi kuibuka wafungaji bora kama ilivyokuwa kwa Boniface Ambani raia wa Kenya lakini raia wa nchi za Afrika Magharibi.
Tchetche amefunga bao moja katika mechi dhidi ya Mgambo JKT wakati Azam FC iliposhinda kwa mabao 3-0.
Kutokana na bao hilo, amefanikiwa kufikisha mabao 17 ambayo hakika si lahisi kufikiwa na mchezaji yoyote.
Ligi hiyo imebakiza mechi moja kwa karibu kila timu huku ambao wanamfuatia ni Didier Kavumbagu wa Yanga na Paul Nonga wa JKt Oljoro ambao kila mmoja ana mabao tisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment