May 12, 2013




Wachezaji Yanga wana kazi mbele yao, uongozi umefikisha dau la Sh milioni 150 kama zawadi ya pongezi kuhakikisha wanaifunga Simba Mei 18.
Awali zilikuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alitenga Sh milioni 10, lakini sasa ameongeza Sh milioni 50 ili Simbaafungwe.

Tayari timu hiyo iko kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo.
“Mwenyekiti (Manji) ameshazungumza na wachezaji na kuwaeleza kuhusiana na suala hilo.


“Amewapa ahadi ya Sh milioni 150, wanachotakiwa wao ni kushinda tu mechi hiyo na si zaidi. Wanalijua hilo na maandalizi yanaendelea,” kilieleza chanzo.
Alipozungumza na Salehjembe, Manji alikiri kuwepo kwa ahadi lakini akakataa kulizungumzia suala hilo.

“Tunachotaka ni ushindi, tayari tumechukua ubingwa lakini tunataka Wanayanga wote washerekee kwa raha zaidi na kuifunga Simba litakuwa ni jambo la msingi.

“Kweli kuna ahadi lakini ni hamasa kwa wachezaji wetu kwa kuwa ndiyo watawakilisha Wanayanga wote uwanjani siku. Hivyo tuiachie hapo,” alisema manji.

Tayari Yanga imebeba ubingwa lakini inaonyesha wamepania kushinda ili kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0 mwishoni mwa msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic