May 25, 2013


Pazi akiwania mpira na Luhende, Yondani wa Yanga


Simba ambayo inataka kurudisha hadhi yake, imefanikiwa kumsaini mshambuliaji wa Ruvu JKT, Zahoro Pazi ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa Simba.

Pazi aliyekuwa akicheza kwa mkopo Ruvu akitokea Azam FC, amemalizana na Simba baada ya mazungumzo ya wiki moja.
Lakini Simba pia imemsajili beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
 
Baba Ubaya akimdhibiti Chanongo wa Simba


Mchezaji wa tatu aliyesajiliwa na Simba ni kipa wa Kagera Sugar, Ntalla.
Pamoja na hivyo, Simba wamefanikiwa kumpa mkataba winga wao Haruna Chanongo.

“Chanongo alikuwa akiwaniwa na timu nyingi ikiwemo Yanga, tayari tumefanikiwa kumpa mkataba,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic