May 18, 2013



Uuzwaji wa tiketi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam umeelezwa kutokuwa katika mpangilio mzuri.
Uuzwaji huo wa tiketi katika magari aina Toyota Hiace umeonekana siyo mzuri na kusababisha vurugu katika maeneo kadhaa.

Mfano, Mbagala kulitokea vurugu kubwa hadi kusababisha gari lililokuwa linauzwa tiketi kuvunjwa vioo.


Inaelezwa, vurugu hizo zilisababishwa na wauza tiketi hao kumruhusu mtu mmoja kununua tiketi 100 za Sh 5,000, hali iliyofanya wengine waingie hofu ya kukosa.

Baada ya kuona hivyo walianza kulaumu wauzaji kumruhusu mtu mmoja kununu tiketi hizo wakiamini angeenza kulangua. Vurugu zikaanzia hapo.


Sehemu nyingine ilikuwa ni barabara ya Uhuru, katika ya jiji ambako kulizuka vurugu kubwa kutokana na utaratibu wa ukataji tiketi kuonekana kutokuwa mzuri.

Mashabiki wa soka wanaonekana kuipania sana mechi hiyo, ingawa wengi wamekuwa na hofu kutokana na kuonyesha utaratibu kutokuwa mzuri tokea mapema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic