Gumzo lilikuwa
ni uchezaji wa Fernando Torres na fedha pauni milioni 50 walizotoa Chelsea
kumhamisha kutoka Liverpool.
Ingawa
ilionekana kama hana msaada, lakini tayari amefanya kazi kubwa kuisaidia timu
hiyo kutwaa makombe mawili makubwa.
Ubingwa wa
Ligi ya Mabingwa msimu uliopita baada ya kuifunga Bayern Munich katika fainali
baada ya kuing’oa Barcelona katika nusu fainali.
Lakini
mchango wake pia umeonekana katika michuano ya Europa League ambayo jana
Chelsea wametawazwa kuwa mabingwa.
Katika
mechi ya fainali, Torres amefunga bao la kwanza lakini amekuwa msaada mkubwa
katika mechi hadi kufikia fainali.
Maana yake
ameifikisha Chelsea kuweka rekodi ya mafanikio makubwa zaidi barani Ulaya
kuliko klabu yoyote.
Hakuna
timu ya England ambayo hata imejaribu kusogelea mafanikio hayo ya kuingia
fainali za Ligi ya Mabingwa na Europa League kwa miaka miwili mfululizo na
kutwaa makombe yote.
Maana
yake, Chelsea hawana sababu ya kujuta kwa Torres ambaye akiwa na timu yake ya
taifa ya Hispania, ameishatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia na ule wa Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment