Kocha Mkuu
wa Taifa Stars ametangaza kikosi kitakachowavaa Morocco Juni 8 mjini Marakesh. Lakini wachezaji wawili makind ndiyo gumzo.
Poulsen
raia wa Denmark amewaita wachezaji kadhaa akiwemo kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’
na makinda wawili kutoka Azam FC na Mtibwa Sugar.
Kocha huyo
amewatema kadhaa akiwemo mkongwe Shabani Nditi wa Mtibwa Sugar.
Kikosi
hicho kitaanza safari kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan mjini Addis
Ababa, Ethiopia Juni 2 kabla ya kwenda Morocco katika mechi hiyo kuwania
kucheza Kombe la Dunia.
Kikosi kamili
hiki hapa:
MAKIPA; Juma Kaseja, Mwadini Ally
Mwadin, Aishi Manula na Ally Mustapha Barthez,
MABEKI; Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Waziri
Salum(Azam), Vicent Barnabas (Mtibwa), Nadir Haroub ‘Cannavaro, Kelvin Yondani
(Yanga), Shomari Kapombe (Simba).
VIUNGO; Mrisho Ngassa, Amri Kiemba,
Mwinyi Kazimoto, Haruna Chanongo (Simba), Simon Msuva, Athuman Idd ‘Chuji,’ Frank
Domayo (Yanga), Khamis Mcha, Salum Abubakar ‘Sure Boy,’ Mudathir Yahaya (Azam).
WASHAMBULIAJIA; Mbwana Sammata, Thomas
Ulimwengu, (TP Mazembe), John Bocco (Azam), Zahoro Pazi (Lyon) na Juma Luizio
(Mtibwa Sugar).
0 COMMENTS:
Post a Comment