Rooney akiwa ukumbini leo, akishuhudia mapambano ya utangulizi |
Mshambuliaji wa Manchester
United, Wayne Rooney amesafiri hadi jijini London kumuunga mkono bondia Carl
Froch.
Rooney aliwashangaza waandishi
baada ya kupitiliza moja kwa moja katika chumba alichokuwemo Froch maarufu kama
Cobra.
Muda huu baadaye, Froch atapanda
ulingoni kuzichapa na Mikkel Kessler katika pambano linalotarajiwa kuwa kali na
la kusisimua katika Ukumbi wa London Arena.
Alipohojiwa, Rooney alisema
amekwenda kumuunga mkono Cobra ambaye ni rafiki yake.
Baba yake mzazi Rooney alikuwa
bondia na katika mahojiano na Sky ukumbini hapo, Rooney alisema baada ya soka
anavutiwa zaidi na mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment