June 2, 2013

Eric Abidal amehitimisha safari ya maisha yake ya miaka sita kwenye kikosi cha Barcelona, ambapo aliagwa kwa hisia kali katika mechi ya mwisho ya timu hiyo, juzi kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Abidal ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33, alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na tatizo la ini aliagwa na kupewa jezi maalum ya ukumbusho.

Mechi hiyo ya mwisho kwa mchezaji huyo ilikuwa katika La Liga dhidi ya Malaga ambapo Barcelona ilishinda mabao 4-1.

Abidal aliyetua klabuni hapo kwa usajili huru akitokea Lyon mwaka 2007, aliingia dimbani kwenye mechi hiyo katika dakika ya 75 na kupata shangwe za nguvu.

Akiwa Barcelona amefanikiwa kutwaa mataji manne ya La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, Copa del Rey mara mbili, Supercopa de Espana mara tatu na Klabu Bingwa Dunia mara mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic