June 3, 2013


Hatimaye Kocha Jose Mourinho, jana usiku aliweka wazi kuwa atatua rasmi kwenye klabu ya Chelsea wiki hii.

Mourinho ambaye anatua klabuni hapo akitokea Real Madrid, ametoa kauli ya kurejea Chelsea rasmi kupitia mahojiano katika kipindi cha televisheni kinachofahamika kwa jina la Punto Pelota.

“Naelekea London Jumatatu (leo) na mwisho wa wiki nitakuwa naanza kazi ya kuwa meneja wa Chelsea. Maisha ni mafupi, unatakiwa uangalie kile kilicho bora kwako,” alisema Mourinho ambaye amewahi pia kuzinoa FC Porto na Inter Milan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic