June 3, 2013

Felix Sunzu mmoja wa wachezaji waliotemwa na Simba.
UONGOZI wa Simba umemaliza kazi ya mchujo wa nyota wake watakaoachwa na sasa kila kitu kipo wazi juu ya panga hilo.
Taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo, zinasema kuwa Simba imechuja nyota nane.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa nyota waliotupiwa virago rasmi na uongozi wa timu hiyo ni Haruna Moshi ‘Boban,’ Ramadhan Chombo ‘Redondo,’ Juma Nyosso, Amir Maftah, Felix Sunzu, Komalmbil Keita, Abdallah Juma na Paul Ngalema.
“Hao wote wanaachwa kwa sababu mbalimbali, mfano kama huyo Nyosso na Redondo kesi yao ni tofauti, hawa wanaachwa kwa kuvunja mikataba yao, yaani sisi kama timu tumeona hatuwahitaji, ingawa bado wana mikataba na klabu,” alisema bosi huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
“Wengine kama Abdallah na huyo Ngalema, hawa nao kuna tofauti kidogo kwa sababu wao binafsi wameomba mikataba yao ivunjwe.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic