BRIAN UMONYI (MBELE) AKIITUMIKIA AZAM FC.. |
Azam FC imewapumzisha kwa mwezi mmoja wachezaji wake wawili,
mshambuliaji Brian Umonyi kutoka Uganda na kiungo Humphrey Mieno raia wa Kenya.
Uamuzi huo unatokana na wachezaji hao kusumbuliwa na majeraha waliyonayo.
Umonyi aliumia vidole vya mguu wa kulia alipokuwa katika timu yake ya
taifa ya Uganda hivi karibuni wakati Mieno ana tatizo la nyama za paja kwa muda
mrefu.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala, amethibitisha kuhusiana na
kupumzishwa kwa wachezaji hao wawili.
“Maandalizi ya msimu mpya yanaendelea kama kawaida na tunaendelea
kusaka mechi za kirafiki kwa ajili ya kujipima.
“Wachezaji wanaonyesha viwango katika kujituma mazoezini na tunaamini
tutakuwa bora zaidi kwenye ligi.
“Ila kuna wachezaji wetu wawili, Umonyi na Mieno, wapo nje kwa muda
kufuatia kuwa majeruhi na tutawaangalia hadi baada ya wiki mbili kuona kama
watakuwa fiti.
“Hatujui kama ligi itakapoanza watakuwa fiti au la kwa kuwa Umonyi
anaumwa vidole vya mguu wa kulia na Mieno anaumwa nyama za paja,” alisema
Ongala.
Azam itaanza Ligi Kuu Bara Agosti 24,
mwaka huu kwa kuwavaa wakali wa Manungu, Mtibwa Sugar ambao watakuwa kwao
katika uwanja uliozungukwa na mashamba ya miwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment