Kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, amerejea kambini
Simba katika Hoteli ya Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
REDONDO (WA PILI KUSHOTO) AKIWA KATIKA BENCHI LA SIMBA PAMOJA NA, KUTOKA KULIA, EMMANUEL OKWI, NKANU BIYAVANGA NA ABDALLAH JUMA...HII ILIKUWA MSIMU ULIOPITA |
Redondo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao hawakumalizia
msimu kufuatia kusimamishwa kwa utovu wa nidhamu.
Lakini amerejeshwa kundini baada ya uongozi kukaa naye na kuzungumza
kuhusiana na matatizo.
Redondo amesema kuwa atajirekebisha kutokana na makosa yaliyotokea
hasa yale ambayo alituhumiwa.
“Nitajirekebisha kwa kile nilichotakiwa kukifanya kulingana na matakwa
ya viongozi wangu na nitakuwa mchezaji mtiifu, sasa nataka kucheza mpira”
alisema Redondo.
Msimu uliopita ulikuwa mbaya kwa Redondo ambaye ni kati ya wachezaji
wenye uwezo mkubwa kama atatulia na kufanya mambo yake kwa mpangilio.
0 COMMENTS:
Post a Comment