Inaonekana kiungo mwenye kasi wa Spurs, Gareth Bale anataka kujiunga na Real Madrid lakini Manchester United wanaoneakana kuwa tatizo kubwa.
The Mirror la Uingereza katika moja ya makala zake limeeleza Bale amekuwa anaonyesha wazi kuwa anataka kwenda Madrid lakini Manchester ni sehemu anayoona ni sahihi.
Bale anaona Man United ni sehemu sahihi kwa maana ya kuendelea kufanya vizuri akiwa nchini Uingereza.
Lakini kama nguvu ya United haitakuwa kubwa, basi atafanya kila linalowezekana kwenda zake Madrid.
Kwani hata wakala wake ameishasema kuwa Bale amekuwa akimueleza nia yake ya kuitumikia Madrid kwa kila hali na ilikuwa ndoto yake tokea akiwa mtoto.
Hata hivyo kocha wake, Andres Villa Boas amekuwa akisisitiza kwamba anataka Bale aendelee kubaki ndani ya kikosi chake.
0 COMMENTS:
Post a Comment