July 24, 2013





Newcastle United ililazimika kupambana na kupata sare bao 1-1 dhidi ya timu ndogo ya Pacos de Ferreira ya Ureno.

Lakini mechi hiyo ilitawaliwa na vituko lukuki likiwemo lile tukio la nahodha wa Newcastler, Fabricio Coloccini kumkaba mshambuliaji Caetano wa Pacos nusura amuue.

Ilionekana kama nahodha huyo alipania kumtoa roho mchezaji huyo ambaye alishindwa kabisa kujitetea kabla ya wengine hawajaingilia kumuokoa.

Mwamuzi alishindwa kujizuia na kutoa adhabu kwa Coloccini ambaye alikasirishwa kupita kiasi na mshambuliaji huyo na inaelezwa kuwa alitoa maneno ya kashfa.

Mshambuliaji Shola Ameobi ndiye alisawazisha bao hilo la Newcastle ambao walionekana wameishafulia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic