Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelo leo amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu hiyo.
Awali Julio alisaini mkataba wa miezi sita ambao ulimalizika wiki iliyopita na jana alipewa mkataba mpya ambao ameusaini tayari.
“Kweli nimeongeza mkataba wa mwaka mmoja na Simba, mambo yanakwenda vizuri na ninaamini titafanya vizuri sana.
“Kikubwa wanachotakiwa watu ni kutuamini makocha wazawa kwamba tunaweza kufanya vizuri,” alisema Julio.
Julio anamsaidia Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment