| MENEJA WA KILIMANJARO, GEORGE KAVISHE AKIWAKABIDHI VIFAA KATIBU MKUU WA SIMBA, EVODIUS MTAWALA (KULIA) NA LAWRANCE MWALUSAKO WA YANGA, KULIA |
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, George Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza
ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila
shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri
ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri.
Ni matumaini yetu kuwa
wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na
kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”
Kilimanjaro Premium Lager kama
mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa
soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu
sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza
wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha
tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.
Kavishe alisema kuwa udhamini wa
Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania,
kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile
kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunawashukuru viongozi wa Simba na
Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano
mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio
ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu.
“Tunawaomba mashabiki wa Simba na
Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani
tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye
kilele cha mafanikio.”







0 COMMENTS:
Post a Comment