Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24
mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo
kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield)
kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu
zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam),
Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal
Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT
Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,
Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi,
Pwani).
0 COMMENTS:
Post a Comment