Mshambuliaji Brenda Ogbu raia wa Nigeria anaonekana kukosa nafasi ya
kuichezea Yanga na huenda akatupiwa virago.
Kumezuka mjadala ndani ya Yanga kwamba Ogbu anaonekana kuwa na
majeruhi ya muda mrefu hali ambayo imewashtua Yanga.
Lakini pia ameshindwa kuonyesha uwezo hata katika mazoezi hivyo
inaonekana hana nafasi.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga kimeeleza Mnigeria huyo
atatupiwa virago na kupewa ruhusa arejee kwao.
“Kulikuwa na mabishano tu kwa kuwa wengine wanataka apewe nafasi zaidi
lakini inaonekana hata benchi la ufundi bado halijaridhishwa naye.
“Hali ilivyo yule Mnigeria tunafikiri ataondoka, yaani hadi sasa ni
asilimia tisini labda itokeaa mtu awashawishi na kubadili uamuzi,” kilieleza
chanzo cha uhakika.
Imeelezwa hata Kocha Ernie Brandts anaonekana kutoridhishwa na kiwango
cha Ogbu ambaye ambaye ana profile kubwa mtandaoni kama mshambuliaji hatari
kutoka Heartland ya Nigeria.
0 COMMENTS:
Post a Comment