Kiungo Mussa Mudde ameingizwa katika kundi la watakaochwa na kikosi
hicho na tayari ameanza mazungumzo ya kulipwa mafao yake.
Taarifa zinaeleza Mudde raia wa Uganda amekubali kuondoka Simba kama
atalipwa mafao yake.
Mwenyekiti wa usajili wa Simba, Zacharia Hans Pope amethibitisha hilo
na kuwataja wachezaji Hamis Buyinza kutoka Uganda na Msudani, Kun kuwa
wametemwa.
“Msudani na beki Mganda wameishaelezwa lakini tuko katika mazungumzo
na Mudde kwa kuwa tulikuwa na mkataba naye ili ikiwezekana tumalizane vizuri,”
alisema.
Mudde ambaye alijiunga na Simba akitokea Sofapaka msimu uliopita
ameshindwa kuonyesha kiwango bora.
Lakini yeye amewahi kusema tatizo lilikuwa ni majeraha aliyoyapata
baada ya kutua nchini na kusisitiza msimu huu ungekuwa wake.
Kama watakubaliana na Simba, maana yake atakuwa ameshindwa kutimiza
ndoto zake za kung’ara akiwa na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment