MABUSELA (KATIKA) AKIKARIBISHWA SIMBA NA MANEMBE
Uongozi wa Simba umeendelea na kufanya majaribio kusaka beki bora wa
kati katika kikosi chake.
Beki huyo Vincent Matsobane Mabusela ametua jijini Dar es Salaam na
kupokelewa na viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
Danny Manembe ndiye alikuwa kiongozi aliyempokea Matsobane kutoka
Black Leopard ya Afrika Kusini.
Kwa umbo si mchezaji mrefu au aliyejaa
kimisuri, hali ambayo inaonyesha hana tofauti kubwa sana na Ssenkoomi raia wa
Uganda ambao mashabiki wa Simba walimkataa kutokana na udogo wa umbo lake.
Akiwa uwanjani hapo, Matsobane
alisema anaijua vizuri Simba pamoja na Yanga kwa kuwa alicheza nazo mechi
wakati timu yake ilipokuja nchini kucheza mechi za kirafiki msimu uliopita.
Akiwa nchini atafanya majaribio na Simba kwa wiki moja au mbili hadi
jibu litakapopatikana.
Tayari Simba imeamua kuwapa nauli Mganda Hamis Buyinza na Msudani Kun,
lakini pia inaonekana safari itawakuta Waganda wawili, Ssenkoomi na Mussa
Mudde.
Simba imekuwa ikihaha kutafuta beki wa kati bila ya mafanikio na Matsobane
hana umbo kubwa, badala yake Simba watategemea kasi na controo ya kutosha.
Matsobane hakuchukua muda mwingi uwanjani hapo alipanda gari na
kuondoka na huenda akaanza mazoezi leo Jumatano.
0 COMMENTS:
Post a Comment