Kiggi (wa tatu kushoto) akiwa na Simba nchini Oman |
Uongozi wa klabu ya Simba
ya jijini Dar umeibuka na kusema kuwa unatarajia kumpeleka nchini India
mchezaji wao Kiggi Makasi.
Kigi amekuwa akisumbuliwa
na goti la mguu wa kushoto kwa muda mrefu ambapo amekuwa akirushwarushwa juu ya
kupelekwa huko.
Akizungumza na Championi
Ijumaa, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema timu ya madaktari wa Klabu
ya Simba wapo katika mchakato wa kusaka ‘appointment’ nchini India ili waweze
kumsafirisha mchezaji huyo.
“Timu
ya kitabibu ya Simba ipo katika mchakato wa kupata “appointment” nchini India
kwa ajili ya kumsafirisha Kigi ili aweze kupata matibabu nchini humo,” alisema
Kamwaga.
Kiggi
aliumia wakati timu hiyo ilipokuwa ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya CDA ya
Dodoma.
Lakini
uongozi wa Simba umekuwa ukisuasua kuhusu kumpatia matibabu kijana huyo aliyejiunga
nao akitokea Yanga.
Kelele
za wadau zimekuwa kubwa kuhusiana na suala hilo na kuutaka uongozi wa Simba
kufanya jitihada.
0 COMMENTS:
Post a Comment