August 9, 2013



Hussein Javu ndani ya jezi aliyokuwa anavaa Kavumbagu.
Didier Kavumbagu.


Na Wilbert Molandi
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Husseni Javu amepewa jezi namba 21 ambayo ilikuwa ikitumiwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo, Mrundi, Didier Kavumbagu.

Javu alijiunga na Yanga hivi karibuni na kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani Morogoro.

Akizungumza na Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema Kavumbagu hataivaa tena namba hiyo, badala yake msimu ujao wa ligi ataonekana akivaa na jezi namba saba ambayo ilikuwa ikitumiwa na Nizar Khalfan.

Saleh alisema kiungo wao mshambuliaji mpya, Mrisho Ngassa aliyetokea Simba amepewa namba tisa iliyokuwa ikivaliwa na Omega Seme aliyepelekwa kwa mkopo Tanzania Prisons.

“Kavumbagu hataonekana akivaa jezi namba 21 kwenye msimu ujao na badala yake ataonekana akivaa namba saba,” alisema Saleh.



1 COMMENTS:

  1. Kavumbagu alianza kuvaa namba 7.raundi ya pili ya ligi kuu ilipoanza msimu ulopita na hata alipoifunga simba alikuwa amevaa namba 7.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic