August 28, 2013





Uzoefu ndiyo umeivutia Simba kumsajili kiungo wake wa zamani, henry Joseph.

Henry amesaini Simba mkataba wa mwaka mmoja akitokea Kongsvinger ya Norway ambayo ilimsajili kutoka Msimbazi.


Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema anaamini kupitia uzoefu wake, Henry atatoa msaada katika kikosi hicho.

“Henry ni mchezaji mwenye uzoefu, anaweza kutusaidia na pia kuwa mfano kwa vijana.
“Suala la atacheza namba ipi, acha tuangalie mazoezi yetu yatakavyokuwa na mwisho tutapata jibu tu,” alisema.

Henry mwenye alisema amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa sharti la kuondoka wakati wowote endapo atapata klabu nje ya nchi.

Henry alisema anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu mara timu hiyo itakaporejea jijini Dar es Salaam ikitokea Arusha inapocheza na JKT Oljoro leo.

“Nimesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu yangu ya zamani ya Simba, baada ya kufikia makubaliano na viongozi wa timu hiyo.

“Katika mkataba huo, tumekubaliana kuwa naweza kuondoka wakati wowote kama nitapata timu nje ya nchi,” alisema Henry.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic