August 21, 2013





Beki kisiki wa kati wa Rhino Rangers ya Tabora, Mbogo Ladislaus ‘Mnyama’, amemwambia mshambuliaji mpya wa Simba, Betram Mombeki, asitegemee mtelemko.

Rhino inatarajiwa kuvaana na Simba katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Ally Hassani Mwinyi mkoani Tabora.
 
 Mbogo amesema hamjui vizuri Mombeki, ila anasikia sifa zake zilizotokana na kufanya vizuri katika michezo ya kirafiki aliyocheza hivi karibuni.

Mbogo alisema kwa kushirikiana na mabeki wenzake, watajitahidi kumdhibiti mshambuliaji huyo aliyewahi kuishi Marekani, ambaye alijiunga na Simba katika kipindi cha usajili kilichopita akiwa mchezaji huru.

 “Maandalizi tunaendelea nayo na tumejiandaa vyema kupambana na wapinzani wetu Simba, kwa upande wa safu ya ulinzi tumejipanga vizuri kukabiliana na washambuliaji wa wapinzani wetu.
“Nasikia wamemsajili mshambuliaji mmoja wa kati ambaye wanamsifia, nasubiri nimuone ndani ya uwanja, nimejipanga vyema kupambana naye,” alisema Mbogo aliyepelekwa huko kwa mkopo na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic