Mshambuliaji mpya wa Simba, Betram Mombeki atakuwa
katika hali nzuri kuichezea timu yake katika mechi dhidi ya JKT Oljoro,
keshokutwa Jumatano.
Mombeki aliumia ugoko katika mechi ya kwanza ya Ligi
Kuu Bara dhidi ya Rhino ya Tabora.
Hali hiyo ilionekana kuzidi kulipa hofu benchi la
ufundi la Simba.
Lakini Daktari wa Simba, Yasin Gembe amesema Mombeki
atakuwa katika hali nzuri kuwavaa wanajeshi hao wa Arusha.
Mombeki alikuwa kati ya wachezaji waliofanya vizuri
katika mechi za kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment