August 22, 2013





Kocha Jose Mourinho wa Chelsea ameanza vituko vyake ambavyo vilikosekana katika Ligi Kuu England kwa miaka kadhaa.

Mourinho raia wa Ureno amemshambuliaji ikiwa ni pamoja na kufikisha mkono wake katika uso wa Kocha Paul Lambert wa Aston Villa.




Makocha hao waliingia katika mgogoro katika mechi iliyokutanisha vikosi vyao jana na Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mourinho alisema Lambert bado ana tabia za kitoto na itafikia wakati atakua na kuachana nazo.



“Hata mimi nakumbuka miaka kadhaa, nilikuwa ninalaumu kila uamuzi wa refa. Itafikia ataacha tu,” alisema Mourinho akilaumu Lambert kutokana na kumlaumu mwamuzi kwamba angetoa penalti wakati John terry alipounawa mpira katika eneo la adhabu.

Mbali na hivyo, Mourinho alikuwa burudani wakati mechi inaendelea kutokana na midadi na namna alivyokuwa akielekeza wachezaji wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic