Kocha Mkuu wa
Uganda, Sredojevic Milutin amesema bado anatafakari kazi kubwa waliyoifanya
kuing’oa Taifa Stars na kupata nafasi ya kucheza michuano ya Chan.
Milutin
maarufu kama Micho amesema haikuwa kazi lahisi kwa kuwa Stars ni timu yenye
uwezo wa juu.
“Unajua watu
wengi wanaona suala hili ni kama dogo au ilikuwa lahisi sana, ila Taifa Stars
ni timu imara sana.
“Kuitoa ni
jambo kubwa kwetu, kwa kuwa ilikuwa changamoto ya juu, imetusaidia sisi kujijenga
zaidi.
“Najua
itatusaidia na mara kadhaa nimekuwa nikiwakumbusha wachezaji.
“Hivi
karibuni tunaingia kambini kujiandaa na mechi za awali kucheza Kombe la Dunia
na ikiwezekana tutaweka kambi nje ya hapa,” alisema Micho.
Kikosi chake
cha The Cranes kiliichapa Taifa Stars kwa jumla ya mabao 4-1, kikianza kushinda
Dar kwa bao 1-0 kabla ya ushindi mnono wa 3-1 mjini Kampala.
0 COMMENTS:
Post a Comment