Usaili kwa wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi
Kuu (TPL Board) unaanza kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
Agosti 30 mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu
pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro na Pwani), kanda
namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es Salaam).
Agosti 31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda
namba saba (Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba
tisa (Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida).
Usaili kwa kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili
(Mara na Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne
(Arusha na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na
Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
Waombaji wote wamepangiwa muda wao wa usaili. Kwa mujibu wa ratiba
usaili ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 2 usiku. Wasailiwa wote
wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment