Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 152,296,000.
Watazamaji 26,137 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare
ya bao 1-1.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa
sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
23,231,593.22.
Mgawo mwingine ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 18,786,827.52, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh.
11,272,096.51, Kamati ya Ligi sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 4,383,593.09.
0 COMMENTS:
Post a Comment