Wachezaji wawili
wa Simba, raia wa Burundi wametua nchini na kukamilisha kikosi kamili.
Kaze Patrick
‘Demunga’ ambaye ni beki wa kati na hahodha wa timu ya taifa ya Burundi na Amis
Tambwe ambaye ni nahodha wa Vital’O wametua nchini tena.
Wachezaji hao walirejea kwao, hata hivyo wamechelewa na kujiunga na Simba ambayo imewasajili kutoka Vital’O.
Tambwe
ndiye mfungaji bora wa michuano ya Kagame na alitoa msaada mkubwa kama ilivyo
kwa Demunga kuisaidia Vital’O kubeba ubingwa wa Kagame huko nchini Sudan.
Wawili hao
walipokelewa na maofisa kadhaa wa Simba ambaye wamekuwa wakifanya kazi hiyo na
mara moja waliwachukua kwenye usafiri wa ‘nguvu’ na kuondoka nao uwanjani hapo.
0 COMMENTS:
Post a Comment