Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti
kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya
Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa walioitwa katika timu hiyo
Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula
(Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe
(Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa
Sugar) na David Luhende (Yanga).
Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum
Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman
Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa
(Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
0 COMMENTS:
Post a Comment