Bondia Phil
Williams aliyedundwa na Francis Cheka katika kuwania ubingwa wa dunia uzito wa Super
Middle unaotambuliwa na WBF ni kinyozi kwao Marekani.
Williams
alipigwa na Cheka baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi Mtanzania huyo
ambaye ameweka rekodi ya kuwa wa tatu kuchukua ubingwa wa dunia baada ya Rashid
Matumla na marehemu Shaaban Magoma.
Mitandao
mbalimbali inaonyesha Williams aliyezaliwa Julai 12, 1977 katika Kitongoji cha
Queens, New York nchini Marekani, amekuwa akifanya kazi kama kinyozi katika mji
wa Minneapolis ambako anaishi kwa sasa.
Pambano kati
ya Cheka na bondia huyo lilikuwa na mvuto zaidi kwa kuwa wawili hao kazi zao za
nje si za ofisini kwa kuwa hata Cheka huuza chupa za plastiki zilizotumika
katika Mji wa Morogoro.
Kabla ya
kupigwa na Cheka kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam,
Williams maarufu kama The Drill, alikuwa amepoteza pambano lake la mwisho kwa
kushindwa na bondia kutoka Poland, Andrzej Fonfara katika raundi ya tatu.
Mmarekani
huyo alionyesha ushindani mkali kwa Cheka ambaye amekuwa bondia Mtanzania
asiyeshindwa katika kipindi hiki, hasa nyumbani.
Taarifa
nyingine zimeeleza, Williams alikuwa akisotea malipo yake kutoka kwa promota aliyeandaa
pambano ambaye pia alikuwa akilia ‘kupigwa’ kutokana na rundo la tiketi feki.
0 COMMENTS:
Post a Comment