Wazee wa
Yanga wakiongozwa na Ibrahim Ally Akilimali wameingia katika mgogoro na uongozi
wa Manji.
Wazee hao
wamefunguka na kusema hawamtaki Katibu Mkuu mpya, Patrick Naggi ambaye anachukua
nafasi ya Lawrence Mwalusako.
Wazee nao
akina Akilimali, Hashim Muhika na Bilal Chakupewa wamesema wazi hawamtambui
Mkenya huyo.
NAGGI |
Katika
Mkutano wao na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa
ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa
na uongozi wa Manji ambayo ni kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri
Katibu mpya kutoka Kenya.
Naggi yupo
tayari nchini kuanza kazi baada ya Mwalusako kuondolewa katika nafasi hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa jhabari klabu leo, Mwenyekiti wa Wazee hao, Ibrahim Akilimali
amesema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, lazima awe mwanachama
wa klabu hiyo, hivyo walivyofanya uongozi ni kinyume kabisa na Katiba
inavyotaka.
“Mpaka sasa
sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama wa klabu
hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na kumpa ushirikiano.
“Kazi za
Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu,
hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu,
tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi,” alisema
Akilimali.
Alisema wao
wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na
anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.
Akilimali
alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi wenye
uwezo wa kushika nafasi hiyo.
“Tunamuona
Mkenya huyu kama ameingia kwa kupitia njia za Panya, kitu ambayo kamwe hatuwezi
kukubaliana nacho,” alisema.
“Kawaida
tumekuwa na kawaida ya kupata taarifa kutoka kwa Manji kama kunakuwa kuna kitu
fulani.
“Huyu mtu
tunamwona ni ‘kanjanja’ aondoke haraka sana, sisi wana Yanga hatumuitaji
kabisa,” alisema Akilimali.
Jana,
Mkenya huyo alikuwa katika ofisi za makao makuu ya Yanga akiwa ameanza kazi na
kufuatilia mambo kadhaa.
Hivi karibuni,
mweka hazima wa Yanga naye aliachia kazi na imeelezwa nafasi yake kushikwa na
mweka hazina huyo mwenye asili ya Kiasia.
Suala hilo
limeelezwa kuigawanya Yanga kwa kiasi kikubwa na huenda likazua mgogoro mkubwa
kama halitafanyiwa kazi haraka.
0 COMMENTS:
Post a Comment