Na Ezekiel
Kamwaga
Klabu ya Simba
ambayo imerejea salama baada mbili za Ligi Kuu Bara katika mikoa ya Tabora na
Arusha na kikosi kpo kamili tayari kujiandaa na mechi ijayo ya ligi dhidi ya
Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyopangwa kuchezwa Septemba 14 mwaka huu.
Kama sehemu
ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja
Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na Mafunzo ya
Zanzibar katika mechi ambayo ina faida nyingine zaidi ya kuwa ya kujiandaa na
mechi ya Mtibwa.
Mosi, mechi
hiyo itatoa nafasi kwa wapenzi na wanachama wa Simba, pamoja na washabiki wa
soka kwa ujumla wake, kupata fursa ya kuwaona kwa mara ya kwanza wachezaji
wapya watatu wa klabu ambao hawajawahi kuonekana wakicheza jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji
hao ni Henry Joseph Shindika aliyetoka Kongsvinger ya Norway, Gilbert Kaze na
Amisi Tambwe waliotoka katika klabu ya Vital’o ya Burundi. Ingawa hawa ni
wachezaji wa Simba lakini hawakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day kama
ilivyo ada kwa wachezaji wote wapya.
Mechi ya
Mafunzo itatoa fursa hiyo ya kutambulishwa na kuonekana wakiitumikia klabu kwa
mara ya kwanza jijini hapa.
Pili, mechi
hiyo itatumika na klabu kwa ajili ya mchezaji wake, Kiggi Makassi, ambaye
atawaaga washabiki rasmi kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini India
anakokwenda kwa matibabu ya goti lake. Kiggi anatarajiwa kuondoka jijini
Septemba tisa mwaka huu.
Kwa vile
Septemba 2 inaangukia siku ya kazi, waandaaji wa pambano hilo wamepanga ianze
saa 11 jioni ili kutoa nafasi kwa wapenzi wengi zaidi kuhudhuria pambano hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment